Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Tanga watakiwa kuendesha shughuli zao kwa ubunifu

Wafanyabiashara Tanga watakiwa kuendesha shughuli zao kwa ubunifu

Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wadogo jijini Tanga wamejengewa uwezo wa kuendesha shughuli zao kwa ubunifu ili wajipatie kipato.

Mafunzo hayo yalitolewa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya biashara uliofanyika juzi Februari 22, 2020.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatatu  Februari 24, 2020 na uongozi wa benki hiyo inaeleza kuwa mafunzo hayo pia yalilenga kuwaongezea uwezo na uelewa katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru amesema wamewajengea uwezo na namna ya kukabiliana changamoto za biashara zao huku akisema huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ni  muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.

 

Amesema  malengo ya klabu za biashara ni  kuwaunganisha na kuwakutanisha wafanyabiashara pamoja ili kutafuta fursa za ufanyaji wa biashara na kubadilishana uzoefu.

Pia Soma

Advertisement
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Maheji ameipongeza NBC hatua hiyo moja ya eneo ambalo wafanyabiashara wengi wanakosa hasa suala la  utunzaji wa taarifa za biashara zao.

“Hatua hii itapunguza  migogoro kati ya wafanyabiashara na Serikali hasa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wakati wa ukadiriaji wa kodi zao,” amesema  Maheji.

Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa TRA ,  Julius Mjenga amesema  wafanyabiashara wanapaswa kuwa makini katika utunzaji wa kumbukumbu za biashara ili kuepusha migogoro  kati yao na mamlaka hiyo.

Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) jijini Tanga, Libera Macha amesema wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali wanaoanza na kuendelea na biashara na kuwataka watu kutosita kwenda kuchukua akisema masharti yake ni nafuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz