Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Soko la Mawenzi walia na faini

Soko La Mawenzi Wafanyabiashara Soko la Mawenzi walia na faini

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa nyanya katika Soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro wamelalamikia kutozwa faini ya shilingi 100,000 na Wakala wa Vipimo, kutokana na wao kutumia kipimo cha ndoo, sado pamoja na mafungu katika shughuli zao badala ya mizani inayotambulika kisheria.

Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko hayo mbele ya Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoani humo Fanuel Mtitu aliefika sokoni hapo kwa ajili ya kuwataka wafanyabiashara hao kuachana na vipimo hivyo vya kiasili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao,wambali na kulalamikia faini hiyo pia wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifanyia marekebisho sheria ya vipimo ambayo wamedai kwao sio rafiki huku pia wakataka elimu zaidi kuhusiana na faini wanazotozwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live