Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara SADC washawishika kuwekeza Tanzania

70579 Brella+pi

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyabiashara katika Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) wamejitokeza kwa wingi katika banda la maonyesho la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini Tanzania (BRELA) kwa lengo la kusajili kampuni na kuwekeza katika viwanda.

Akizungumza na Mwananchi jana Alhamisi Agosti 8, 2019 Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ikiwa ni siku ya mwisho ya maonyesho ya bidhaa katika wiki ya viwanda kwa Nchi 16 za jumuiya hiyo, Mwandamizi Msajili msaidizi, Angela Kimario alisema tangu kuanza kwa maonyesho hayo wamejitokeza wageni kutoka Zimbabwe, Afrika Kusini na Malawi.

“Jana (juzi) nilipokea wafanyabiashara wa Malawi, Afrika Kusini watatu na wengi walikuwa wafanyabiashara wa Zimbabwe, baada ya maelezo yetu wameonyesha nia ya kuja kuwekeza katika viwanda na kusajili kampuni, takwimu sina kwa sasa,” alisema Angela.

Hata hivyo, Angela alisema sheria mbili; sheria ya kampuni ya mwaka 2002 na Sheria ya Taifa ya Viwanda inayohusika na usajili na utoaji wa leseni ya mwaka 2002 hazijaweka vipaumbele kwa nchi 16 za Jumuiya hiyo

“Kwa hiyo taratibu za kusajili kampuni zinabakia kuwa zilezile kwa yeyote anayetoka nchi za SADC au ndani ya SADC, kazi kubwa inafanywa na watu wa Kituo cha uwekezaji , hao ndiyo wanaweza kuwa na vipaumbele zaidi katika eneo hilo,” alisema Angela.

Chanzo: mwananchi.co.tz