Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Mtwara waitwa Comoro

4963b94ff571cb588f00cb30cf6148ea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Marko Gaguti

Mon, 16 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Marko Gaguti amewataka wafanyabiashara wa Mtwara na mikoa mingine nchini Tanzania kuchangamkia fursa za biashara, ambazo kwa sasa zipo nchini Comoro.

Gaguti ametoa wito huo leo Jumatatu Mei 17, 2022, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake aliyoifanya nchini Comoro, kuangalia bidhaa na huduma za Tanzania ambazo ambazo zipo nchini humo.

Gaguti amesema Comoro wana uhitaji mkubwa wa bidhaa mbalimbali hasa za chakula kuanzia mchele, maharage, nyama, karanga ,ulezi na ufuta.

"Baada ya kwenda Comoro tumeridhika kwamba kuna fursa kubwa za kibiashara kati yetu na Comoro, hasa biashara za chakula au bidhaa chakula za viwandani," amesema.

Amesema mahitaji ni makubwa zaidi kwenye bidhaa za nyama, ambapo nchi hiyo inahitaji kotena 20 kwa mwezi pamoja na kotena saba za nyama ya kuku na kontena za mayai kwa mwezi.

Amesema serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine, wanafanya jitihada kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro wanakuwa na ushirikiano mzuri, kwenye biashara hizo ikiwemo kuhakikisha kunakuwepo na usafiri wa bidhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live