Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Mbagala watakiwa kuwa wavumilivu

Mbagz Soko la Mbagala rangi tatu liliteketea siku mbili zilizopita.

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtinika amewataka Wananchi na Wafanyabiashara ambao mali zao ziliteketea kwa moto katika soko la Mbagala rangi tatu mnamo usiku wa kuamkia Feb 13, 2022 kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho wanasubiri majibu ya chanzo cha moto huo kutoka katika Kamati ya uchunguzi iliyoundwa kuchunguza jambo hilo.

Mtinika pia amewataka Wafanyabiashara hao kutokujenga wenyewe soko hilo bali wasubiri maelekezo na Halmashauri itatoa fedha za kukarabati baada ya ripoti ya chanzo cha moto kujulikana na kujadiliwa katika vikao vya Halmashauri.

Mtinika ametoa kauli hiyo alipokutana na Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katika Soko hilo leo mchana alipokwenda kwa ajili ya kuwapa pole kutokana na janga hilo.

"Kama Uongozi wa Halmashauri tunasubiri taarifa ya uchunguzi wa Kamati ukamilike tuwaahidi tu kuwa tutafanya ujenzi wa haraka wa soko hili ili kuruhusu Wananchi kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live