Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Makumbusho wahofia stendi kuhamishwa

Makumbusho Stand Wafanyabiashara Makumbusho wahofia stendi kuhamishwa

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema stendi ya makumbusho haitahama kwenda stendi mpya ya Mwenge badala yake utawekwa utaratibu maalum, ili stendi zote zitumike kikamifu.

Kauli hiyo ya Chalamila imekuja mara baada ya mfanyabishara Samora Wiliam maarufu kama Big kuuliza hatima ya wafanyabishara wa Soko la Makubusho, Dar es Salaam, baada ya stendi hiyo kuhamia Mwenge.

"Soko la Makumbusho ni bega kwa bega na stendi ya Makumbusho na tunasikia za chini chini kuwa stendi hii ya Makubusho inahama baada ya stendi ya Mwenge kukamilika, sasa hizi biashara tunategemea magari zitakapohama biashara zitayumba, tunaomba hilo liangaliwe,"ameeleza Big.

Akijibu hoja hiyo Chalamila amesema hakuna mpango wowote wa kuondoa magari katika Stendi ya Makubusho na kusisitiza kuwa magari yatakuwa yakiingia na kutoka katika stendi zote.

Amewatoa hofu kwa kusema wataweka utaratibu maalum wa magari kuingia na kutoka katika stendi zote, ikiwemo yale magari yenye ruti ndefu. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live