Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Majimoto wamsagia kunguni ofisa TRA

TRA Wafanyabiashara Majimoto wamsagia kunguni ofisa TRA

Sun, 18 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAFANYABIASHARA wa soko la Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kumuondoa Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Majimoto Fraseck Mwakalenga kwa madai ya kukusanya kodi kiholela ikiwemo matumizi ya lugha za kuudhi.

Wakizungumza mbele ya Meneja wa (TRA) Mkoa wa Katavi Nicholaus Migera wamesema kuwa wamechoshwa na vitendo vya kukadiliwa kodi kubwa kinyume na mapato ya biashara zao, jambo ambalo limepelekea baadhi yao kufunga biashara.

Aidha wameongeza kwa kusema kuwa kwa muda mrefu wakihoji kuhusu jambo hilo wamekuwa wakijibiwa kuwa ambaye haridhiki na makadirio hayo au faini zinazotozwa na mamlaka hiyo afunge biashara.

Akijibu tuhuma hizo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi Nicholaus Migera amewaomba radhi wafanyabiashara hao kwa changamoto walizopata na kuahidi kuwa mamlaka hiyo inayafanyia kazi changamoto zote zilizo elezwa ili kukuza ustawi wa biashara na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.

Migera amesema Mamlaka hiyo itaendelea na program ya elimu kwa mlipa kodi ili kukuza uelewa wa masuala ya kikodi kwa wafanyabishara pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wake ili kujiepusha na ukiukwaji wa maadili wakati wa ukusanyaji wa kodi na tozo zingine kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live