Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Kariakoo wavurugana

Kariakoo 3 Pichnjj Wafanyabiashara Kariakoo wavurugana

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya wafanyabiashara kukubaliana kufunga maduka katika soko la Kariakoo, baadhi wanatofautiana na msimamo huo wakieleza kuwa wanategemea biashara kuendesha maisha yao.

Uamuzi wa kufunga maduka umetangazwa leo na viongozi wa wafanyabiashara muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa Amos Makalla kuondoka, wakidai watafungua baada ya kuwa wameonana Rais Samia Suluhu Hassan.

Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa watakaobainika kufungua biashara zao katika soko hilo, wasije kulaumu pale litakapo wakuta jambo, japo haikubainishwa ni jambo gani hilo litawatokea wale watakaokwenda kinyume na msimo huo.

Muuzaji wa nguo za kike maarufu (Madera) Ester Nickson amesema ni kweli kuna matatizo mengi kwenye soko hilo lakini ni vyema wakati mwingine busara ikatumika.

Amesema mkuu wa mkoa ameongea vizuri kwa hatua za awali wangemsikiliza na kumpa muda kama alivyosema anaenda kuongea na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Mimi binafsi siafikiani na mgomo huu, mfano nimeingiza mzigo kwa mkopo, natakiwa kuuza ili nirejeshe mkopo mbaya zaidi ninaoda za watu," amesema Ester

Mfanyabiashara mwingine Mudrick Hafidh amesema hakubaliani na mgomo huo na kwamba waangeacha wanaotaka kugoma wagome na wale wanaaotaka kufanya biashara, waachwe wafungue maduka yao.

"Ni watu wachache wanafanya biashara kwa mitaji yao, wengi wamekopa kufunga biashara siku moja ni hasara kubwa unapata, watu wanaoda za watu ukionekana hata unaitoa ni vurugu," amesema Hafidh

Chanzo: www.tanzaniaweb.live