Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Kariakoo: Tumevurugwa sana na TRA

Kko Mgomoooo Wafanyabiashara Kariakoo: Tumevurugwa sana na TRA

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa Kariakoo Dar es Salaam wamegoma kufungua maduka leo huku wakitaka kuonana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumueleza kero zao ikiwemo utitiri wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wakiongea leo mbele ya Waandishi wa Habari wamedai kwamba lengo la kuonana na Rais ni kumueleza juu ya Kodi, ukamatwaji holela na matumizi ya mashine za EFD.

Mmoja wa Wafanyabiashara amenukuliwa akisema “Uje hapa mbele yetu utupe panadol tumevurugwa mno na TRA na wanaongea vizuri mno, ukikutana na Meneja wa Elimu ya Mlipa Kodi ana maneno mazuri mno lakini pakikucha tu asubuhi Vijana wake hawa hapa”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live