Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Iringa wagoma kisa bomoabomoa

Iringa Wafanyabiashara Mgomo Wafanyabiashara Iringa wagoma kisa bomoabomoa

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara katika eneo la Miyomboni, Manispaa ya Iringa wamegoma kuendesha biashara zao wakilalamikia zoezi la bomoa bomoa ya vibanda vya baishara linaloendelea kwenye eneo hilo.

Tangu alfajiri leo, Juni 15, 2023 wafanyabishara hao waliweka kambi katika eneo la Stendi Kuu ya zamani kujadili suala hilo.

Awali, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa iliendesha shughuli ya kuwahamisha wafanyabishara wadogo maarufu kwa jina la machinga toka katikati ya mji hadi Mlandege ambako, limejengwa soko kwa ajili yao.

Tangu jana Juni 14, 2023 baadhi ya mgambo waliendelea kubomoa vibanda katika eneo la stendi kuu ya zamani jambo lililowafanya leo alfajiri wakutane na kuamua kufanya mgomo.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego tayari amesitisha ubomoaji huo jambo lililosababisha wafanyabishara hao warejee kazini na kufungua maduka yao kama kawaida.

Wakizungumza na Mwananchi, baadhi ya wafanyabishara hao walisema kinachofanyika ni uonevu kwani licha ya kubomolewa maeneo yao wamekuwa wakiharibiwa baadhi ya bidhaa zao.

“Tunaomba kusaidiwa, hii hali sio ya kawaida kabisa kwa nini wanaendelea kutusumbua tena wanakuja huku wakiongozana na polisi,” alisema Yasin Kuliva, mmoja wa wafanyabishara.

Awali Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara wa Mkoa a Iringa, Kola Mtende alisema jana kulikuwa na taharuki iliyosababisha baadhi ya wafanyabishara kupata hasara kubwa.

“Toka jana watu wamekuwa wakishauri na kupendekeza tufanye mkutano hata usiku, na sisi baada ya kukaa na kujadiliana tukalazimika kuwa na mkutano wa dharura leo asubuhi nini tufanye kutokana na hii taharuki ya kubomolewa maeneo yetu,” alisema

Dendego alitangaza kusitisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Jumuiya ya Afanyabishara ya Mkoa wa Iringa na Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuketi kwenye meza moja ya mazungumzo.

“Nalisitisha zoezi ili nitoe nafasi uongozi wa wafanyabishara na manispaa wafanye tafiti na kutoa mapendekezo,” alisema Dendego na kuongeza;

“Kwanza niombe radhi kwa hii kadhia, niwape pole walioumia na sisi tutachukua hatua. Yapo maelekezo mahususi tuliyotoa na utekelezaji wake ndio umeleta kadhia hii. Tutapita kwa wenzetu wote waliopata kadhia hii tuone walichofanyiwa ni sahihi au sio sahihi,” amesema Dendego.

Amesema anaamini kila mmoja atatibiwa kulingana na jeraha alilopata na kusisitiza “ Mtuachie wale walioguswa direct lakini wale ambao hawajaguswa warudi wakaendelea,”

Amewahakikishia wafanyabishara hao kuanzia muda aliotoa tamko hilo, hakuna jambo la hovyo hovyo litakalotokea baina ya wafanyabishara na Serikali kwenye wilaya yoyote.

“Jambo lolote tunaposhindwana tukae tuzungumze, niwaambie Serikali yetu ipo na sisi, katibu waruhusu wafanye biashara wafungue maduka,” amesema Dendego

Chanzo: www.tanzaniaweb.live