Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Geita Waanza Kustawi Kupitia GGML

1 5?fit=700%2C354&ssl=1 Wafanyabiashara Geita Waanza Kustawi Kupitia GGML

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Imeelezwa kuwa marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanywa na Bunge mwaka 2018 na 2019, yameanza kuwanufaisha wafanyabiashara wa Kitanzania kupata fursa za kibiashara kwenye makampuni makubwa ya madini nchini.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kampuni ya Geita Gold Mine Ltd- (GGML) kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi – (NEEC) kutoa mafunzo ya usimamizi wa biashara kwa wafanyabiashara 320 mkoani Geita yaliyowawezesha kushinda zabuni mbalimbali ndani ya kampuni za uchimbaji wa madini mkoani humo.

Kutokana mafunzo hayo Kampuni mama ya AngloGold Ashanti kupitia GGML hivi karibuni imetoa kandarasi ya miaka miwili ya usafirishaji wa mafuta, yenye thamani ya takriban dola za Marekani milioni 10.8 kwa mwaka, kwa wakandarasi wawili wa Tanzania.

Miongoni mwa kampuni zinalizofaidika ni Blue Coast Investment Limited, kampuni ya Geita ambayo inashughulika na usafirishaji, uhifadhi wa mizigo mbalimbali.

Akizungumzia fursa ambazo kampuni hiyo imepata baada ya kupatiwa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Ndahilo Athanas  alisema mbali na kuongeza ubora wa huduma wanazotoa pia mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza idadi wa wateja.

“Ninashukuru kampuni ya GGML kutekeleza sheria za ndani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunda mazingira mazuri ya biashara kwa kampuni za hapa nchini.

“Hapo awali, Blue Coast Investment Limited ilijitahidi kupata fursa za biashara kutoka kwa kampuni za madini zinazofanya kazi huko Geita lakini kushinda zabuni ya usafirishaji wa mafuta inatokana na marekebisho ya Sheria ya Madini pamoja na mpango wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wazalendo  ambayo yalifadhiliwa na GGML.

“Mafunzo haya yameleta matokeo chanya. Tulijifunza mengi ikiwa ni pamoja na kufuata vigezo muhimu vya usambazaji wa bidhaa na utoaji huduma kwenye makampuni ya madini na sekta zingine.

“Baada ya kusoma tangazo kwenye gazeti kuhusu zabuni hii ya usafirisha mafuta kwa miaka miwili, niliamini kampuni yangu inastahili nafasi hii. Ilitoa fursa ya kipekee kwetu kuwasilisha andiko let una kushindana. Tuna bahati kuwa kati ya kampuni mbili zilizoshinda zabuni hii,” alisema Ndahilo.

Programu maalum ya kujenga uwezo wafanyabiashara wa mkoa wa Geita imeongeza uwazi wa viwango vya ununuzi wa biashara ya GGML na kufanya iwe rahisi kwa wafanyabiashara wa ndani kuwa mmoja wa wasambazaji wa bidhaa ndani ya kampuni kubwa ya madini nchini.

Kupitia mafunzo hayo hadi sasa wafanyabiashara 320 wamepata mafunzo huko Geita na wafanyabiashara 50 wapo katika michakato ya tathmini ya kupata mikataba ya usambazaji.

NA MWANDISHI WETU

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz