Jumla ya wafanyabaishara wapatao 40 kutoka Nchini DRC wameitembelea miradi mbalimbali ya kimkakati Nchini Tanzania kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali za kiuwekezaji na usafirishaji kupitia ushoro wa kati.
Akizungumza baada ya ziara hiyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Tax amesisitiza juu ya ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na DRC katika kukuza uchumi , na kuwasihi wafanyabiashara hao kuendelea kutumia bandari ya dar es salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa biashara kutoka Shirika la Reli Tanzania TRC bwana Diamon Mwakaliku amesema kuwa ujio wa wafanyabaishara unamaama kubwa sana kwa shirika hilo kwani Tanzania ni lango la kuingiza mizigo kupitia bandari ya Dar es salaam na kwenda katika nchi za ushoroba wa kati zikiwemo nchi za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda jambo ambalo linazidi kuonesha umuhimu wa miradi kama SGR.