Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau watakiwa kuvisaidia vyuo vya utalii

15746 Pic+utalii TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Wadau wa utalii wilaya ya Serengeti, Mara wametakiwa kuvisaidia vyuo vya utalii ili kuzalisha vijana wenye weledi watakaopata ajira kwa urahisi katika hoteli na kambi wilayani humo.

Akizungumza leo Septemba 4, mwakilishi wa mkurugenzi wa kampuni ya Singita Grumeti Reserves Ltd, Graham Ledge amesema wao kama wawekezaji wana wajibu mkubwa kusaidia Chuo cha Utalii Serengeti ili kuzalisha vijana wazuri watakaoingia kwenye soko la ushindani la utalii.

Ledge amesema kampuni yao inapata shida kupata vijana wenye weledi kwenye eneo la utalii.

Kampuni hiyo imetoa msaada wa jiko la kutengeneza mikate lenye thamani ya Sh450,000 ili kuwasaidia  wanafunzi wa Chuo cha Utalii Serengeti kujifunza vyema mapishi.

Amesema kutokana na uchache wa vijana wenye taaluma hiyo, wanalazimika kuajiri na kuwafundisha tena.

Mkuu wa Chuo cha Utalii Serengeti, Samwel Peter amesema msaada wa mashine hiyo utarahisisha utoaji  mafunzo kwa vitendo na kuongeza wahitimu wenye sifa stahiki katika soko la ajira.

"Hapa watajifunza maarifa mbalimbali yatakayowasaidia kujiajiri na kuajiriwa, tunaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia ili kuzalisha vijana watakaoingia kwenye soko la ajira kwa urahisi," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz