Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wataka teknolojia zaidi kilimo cha mashamba makubwa

Chai Ed Wadau wataka teknolojia zaidi kilimo cha mashamba makubwa

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), Dk Rashid Suleiman amesisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia kwenye kilimo cha mashamba makubwa ili kuongeza tija kwenye kilimo hicho.

Dk Suleiman amebainisha hayo jana Machi 20, 2023 kwenye mjadala ulioandaliwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini ukiwa na mada isemayo “nini kifanyike kuwezesha wanawake na vijana kulisha dunia kupitia kilimo”.

Amesema tafiti pia zifanyike ili kuchochea uzalishaji ambao utakuwa wa manufaa kwa vijana na wanawake ambao wamebaki nyuma katika sekta hiyo.

“Sasa ni wakati wa kuanza kutumia teknolojia kwenye kilimo ili kupiga hatua mbele kama ilivyokusudiwa. Pia, tafiti zifanyike za kutosha ili vijana wazalishe kwa tija,” amesema mwanazuoni huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live