Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wataka juhudi kuongeza uwakilishi wanawake katika soko la hisa

Uchumi Kupanda Wadau wataka juhudi kuongeza uwakilishi wanawake katika soko la hisa

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Soko la hisa imetajwa kuwa miongoni mwa sekta zenye uwakilishi mdogo wa wanawake wanaoshika nafasi za juu kuziongoza taasisi hizo.

Imeelezwa kuwa kati ya asilimia 21 ya wanawake wanaoshika nafasi za juu kwenye taasisi mbalimbali nchini, ni asilimia 14 pekee wenye nyadhifa hizo kwenye soko la hisa.

Akizungumza jana, Machi 8, 2023 katika hafla ya Ring the Bell iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Mary Mniwasa amesema kuna haja ya kuongeza juhudi za kufikia usawa.

"Hili ni eneo muhimu katika sekta ya fedha, pamoja na maendeleo yaliyopatikana lakini uwakilishi wa wanawake ni mdogo katika nafasi za juu za uongozi.

"Ni asilimia 21 ya wanawake wanaoshika nafasi za juu katika sekta ya fedha, lakini ni asilimia 14 pekee hushika nafasi hizo kwenye soko la hisa," ameeleza.

Hali hiyo, amesema ndiyo iliyoonyesha haja ya wadau zaidi ya 100 kutoka serikalini na sekta binafsi wakutane katika hafla ya Ring the Bell.

Amefafanua hafla hiyo iliyoharibiwa na DSE, na UN-Women kwa ufadhili wa Stanbic Bank na TTCL imelenga kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uchumi na kudumisha maendeleo endelevu.

Katika hotuba yake akimwakilisha Waziri WA Viwanda na Biashara, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifah Hamis amesema kuna haja ya kufanyika juhudi za kuhakikisha wanawake wanafikia teknolojia za kidigitali.

“Hii inahusisha kuondoa ombwe la wanawake katika digitali na kuhakikisha wasichana na wanawake wanazifikia teknolojia hizi na wanasaidiwa kupata ujuzi na uelewa wa digitali," amesema.

Hata hivyo, ameeleza umuhimu wa elimu kwa wanawake ili wanufaike sawa na teknolojia za kidigitali ukizingatia Serikali inawekeza nguvu katika eneo hilo.

Chanzo: mwanachidigital