Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wakumbushwa kuunganisha nguvu kuzalisha mazao ya viungo

The Story Of Spice 2 Wadau wakumbushwa kuunganisha nguvu kuzalisha mazao ya viungo

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Kilimo imesisitiza umuhimu wa wadau kuunganisha nguvu katika kuimarisha uzalishaji wa mazao ya viungo kulingana na mahitaji ya soko.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Machi 25 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dk Musa Ally Musa kwenye mkutano wa mamlaka za kudhibiti mazao ya nafaka na mchanganyiko kutoka halmashauri za wilaya, kampuni zinazosindika viungo na asasi za kiraia.

Musa amesema Mkoa wa Morogoro una fursa za kuzalisha mazao ya karafuu, mdalasini, iliki na mchaimchai ambayo yana soko la uhakika na bei yake ni nzuri.

New Content Item (1)

Akitolea mfano mwaka jana, amesema Halmashauri ya Morogoro ilizalisha tani 2,000 za karafuu zenye thamani ya Sh36 bilioni.

Amesema hali ya hewa na ardhi ya mkoa huo ina rutuba ya kutosha jambo linaloibua fursa za kuzalisha mazao mengi ya viungo.

Hata hivyo, wakizungumza katika mkutano huo, baadhi ya wadau wameitaka Serikali kutengeneza sera rafiki ya kukuza, kuzalisha na kusindika viungo kwa lengo la kutafuta soko zuri zaidi ndani na nje ya nchi.

Wamesema uwapo wa sera hiyo, utasaidia pia kuwaongoza wakulima watakaojikita kwenye kilimo cha mazao ya viungo.

Juliana Moses, mkulima wa karafuu ameshauri uwepo wa ubia wa kuwawezesha wadau katika sekta ya viungo kubadilishana maarifa, mbinu bora na uvumbuzi wa changamoto katika uzalishaji, usindikaji na uuzaji.

“Ninapozungumzia ubia, nataka ukiundwa uendeshwe kwa ufanisi na uwazi ili tufikie lengo na kutengeneza adidu za rejea,”amesema Moses.

Meneja wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Njanda ya Juu Kusani mwa Tanzania (Sagcot) Kongani ya Kilombero, John Nakei amesema kituo hicho kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na wadau wa kilimo, wamejipanga kuona mpango huo unafanikiwa.

"Tumejipanga vizuri kuhakikisha karafuu inazalishwa kwa wingi na ubora ule ule ikiwamo kutoa mafunzo kwa wakulima na maofisa ugani," amesema Nakei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live