Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau waiomba Serikali kushusha bei mashine za ETS

ETS MASHINE Wadau waiomba Serikali kushusha bei mashine za ETS

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wenye viwanda nchini wameiomba Serikali ipunguze gharama za stempu za kielektroniki (ETS). Ombi hilo linakuja huku Kamati ya Maboresho ya Sera za Kodi inayohusika na matayarisho ya Bajeti IRA.

Serikali ikikaribisha wadau kutoa maoni yao kuhusu bajeti ya mwaka 2022/2023. Kamati hiyo itaanza kazi yake Februari 2022 hadi Februari 10 na itapokea maoni ya wadau, kufanya uchambuzi na majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusu sera za kodi na usimamizi wake.

Akielezea matamanio yao katika mwaka mpya wa fedha ujao, Mtaalamu wa Sera wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Frank Dafa alisema kuwa ETS inaongeza gharama za kufanya biashara hivyo jambo hilo linapaswa kutazamwa upya.

"Tunafikiri sasa Serikali italian-galia upya hill suala la ETS. Hata kama sio kuondoa utaratibu huo, basi kupunguza gharama zake kwa sababu zilizopo sasa zinakwaza biashara," alisema.

Dafa aliitaka Serikali kuweka ulinzi wa kikodi kwa viwanda vya ndani na kutoza kodi kubwa kwa bidhaa za nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live