Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau waijadili sera ya huduma ndogo za fedha

18020 Pic+fedha TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema sera ya huduma ndogo za fedha imeweka mazingira ya kuchochea ubunifu kukidhi mahitaji ya wananchi wa kipato cha chini ili kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini.

Akifungua mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya fedha nchini unaojadili utekelezaji wa sera hiyo ya mwaka 2017 leo, Septemba 18, 2018, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Katibu Kazungu amesema: "Utaratibu wa kukutana utasaidia kuboresha utendaji wa sekta ndogo ya fedha na ni hatua itakayochangia ukuaji wa uchumi nchini wa viwanda na kupunguza umasikini."

Amewataka wadau wote kujadili kwa kina fursa zilizopo kwenye sekta ya huduma ndogo za fedha na kuainisha maeneo ya vipaumbele yanayopaswa kufanyiwa kazi kati ya mwaka huu wa fedha hadi 2019/20.

Chanzo: mwananchi.co.tz