Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wa usafiri watakiwa kutoa maoni kuboresha usafiri ardhini

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) imekutana na wadau mbalimbali wa usafirishaji kwa ajili ya kutoa maoni yao ili kuboresha rasimu za kanuni mbalimbali zitakazotumika katika uendeshaji wa mamlaka hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 26, 2019 katika ufunguzi wa kikao hicho mkoani Mwanza nchini Tanzania,  Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe amesema lengo ni kuboresha na kuinua sekta ya usafirishaji.

"Hatua hii inalenga kutoa maoni kuhusu kanuni hizi  kabla hazijaanza kutumika," amesema

Wadau hao ni pamoja na wawakilishi wa  madereva magari ya mizigo, waendesha bodaboda, teksi, bajaji na mabasi ya abiria.

Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Christopher Kadilo amewasisitiza washiriki hao kuwa huru kutoa maoni yao.

Amesema kumekuwapo na utaratibu wa baadhi ya watu kuona aibu kutoa maoni yao halafu zikishapitishwa kanuni au sheria wanaibua malalamiko baadaye.

Pia Soma

"Tusiishie kuwa wataalamu tu, tutoe maoni yetu badala ya kusubiri kulalamika baadaye, kila mwenye wazo lake ahakikishe anayatoa hapa ili yafanyiwe kazi," amesema.

Amesema jumla ya kanuni nane zitawasilishwa na kutolewa maoni kwa wadau hao ikiwa ni pamoja na kanuni ya kuyatambua magari ya biashara na madereva, magari ya mizigo, ada za madereva na ukodishwaji wa magari.

Nyingine ni tozo mbalimbali za magari, kushughulikia malalamiko mbalimbali,

Chanzo: mwananchi.co.tz