Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wa Tanzanite kukutana kujadili zuio la utoaji madini ghafi

Wadau wa Tanzanite kukutana kujadili zuio la utoaji madini ghafi

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mirerani. Wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kesho watakutana na viongozi wa Tume ya Madini ili kujadili zuio la madini ghafi kutotolewa nje ya ukuta wa Tanzanite bila kuongezewa thamani.

Mkutano huo utahusisha maofisa wa tume ya madini, wamiliki wa migodi, wachimbaji, wanunuzi, madalali, wachakataji, wafanyabiashara na wadau wa madini.

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akihojiwa na Mwananchi Digital leo Oktoba 28, 2019 amesema kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kesho Oktoba 29,2019 kwenye ofisi zao zilizopo mji mdogo wa Mirerani.

Ntalima amesema lengo la mkutano huo ni majadiliano shirikishi kwa ajili ya kupata ufumbuzi kwenye agizo la zuio la kutotoa madini ghafi ndani ya ukuta ifikapo Novemba mosi.

Amesema wadau hao watakutana kujadili tangazo hilo la ukomo wa kutoa madini ghafi ya Tanzanite bila kuongeza thamani.

“Mkutano huo ni muhimu ili baadaye kusiwe na minong’ono, lawama na kushutumiana hivyo wajitokeze kwa wingi kutoa maoni, ushauri na mapendekezo yao juu ya hilo,” amesema.

Pia Soma

Advertisement

Hivi karibuni Ntalima alitoa tamko la Serikali la kuongeza thamani ya madini hayo ifikapo Novemba Mosi, mwaka huu.

Ntalima amesema muda huo ukifika, madini hayo hayataongezwa thamani, yatahifadhiwa hadi yaongezwe thamani.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji Mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo amesema bado mazingira siyo rafiki katika kuanza kwa mpango huo.

Ofisa habari wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini (Femata) Dk Bernard Joseph amesema Serikali inapoanzisha jambo lake huwa imekuwa imejipanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz