Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau mifugo wajadili rasimu ya mkataba wa huduma

2fa3f72f046ef1383fdb249fc5932b62 Wadau mifugo wajadili rasimu ya mkataba wa huduma

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wa sekta ya Mifugo na Uvuvi wamekutana jijini Dodoma kutoa maoni kuhusu rasimu ya mkataba wa huduma kwa wateja.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa kutoa maoni kuhusu rasimu hiyo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Mhina alisema mkataba huo ni muhimu kwani unawasaidia kwenye weledi.

“Tunatakiwa kwenda katika misingi ambayo inazingatia kanuni za utumishi wa umma, sambamba na uadilifu, weledi na uwajibikaji. Kwenye eneo la weledi ni lazima kuwe na viwango vya huduma bora kama taasisi ndipo pale tunapopambanua kuwafikia wateja wetu kila kundi lina matarajio yake.

“Ukiwa shambani kwako tunakuhudumia kwa huduma za ugani, tunahakikisha tunakufikishia kwa wakati na kwenye mifugo hivyohivyo. Hata kwenye masoko tunafanya hivyohivyo pamoja na huduma za vibali haya yote yanagusa katika weledi,” alisema.

Dk Mhina alisema matarajio ya serikali na wizara ni kufikia malengo ya kutoa huduma bora ambazo zitaleta mabadiliko makubwa.

Kwa upande wake Ofisa Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wamoja Ayubu ambaye pia ni mratibu wa rasimu ya mkataba kwa mteja alisema mkataba huo unaelezea namna ambavyo mteja anaweza kurejesha mrejesho wa huduma ambayo ameipata na hivyo kuwa na nafasi ya kupima utendaji wa taasisi na wateja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live