Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau maendeleo kujadili sera na tafiti za sekta binafsi leo DSM

08fcc9d6a4437808d779a84ff8c87f10 Afisa Mawasiliano Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo Tropiki (IITA) Bi. Catherini Njuguna

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dar es salaam leo hii, itakuwa mwenyeji wa mkutano wa wadau wanaojihusisha na Utungaji wa sera, Watafiti, sekta Binafsi na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuchukua hatua madhubuti zinazohitajika ili kuendeleza na kukuza sekta endelevu nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Bi. Catherini Njuguna kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) nchini Tanzania ambaye pia ni Afisa Mawasiliano Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo Tropiki (IITA) mapema jana alisema tukio hilo litafunguliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, ambapo washiriki watakutana kujadili masuala muhimu ya kimaendeleo kutoka kwa watunga sera na wadau.

Amesema tukio hilo la kisera litakutana na wadau ili kupeana Maarifa,Matokea, na kuangalia sehemu muhimu zenye tija zinazotokana na tafiti za kila siku kwa kuangalia athari za kimazingira nchini ambazo zinahusisha maamuzi na utungaji wa sera.

"Mjadala mkubwa utakuwa ni kuongeza uelewa juu ya masuala muhimu ya kimazingira na kuzikabili changamoto wanazokumbana nazo wadau wadogo ambao wanajihusisha na uzalishaji wa kila siku mpamoja na kuwakutanisha na wadau wakubwa wa kimaendeleo nchini Tanzania." Alisema Catherine.

Tukio hilo ni sehemu ya mfululizo wa mafunzo ya ufugaji na mabadiriko ya Tabia nchi ambazo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara na wadau wa mazingira ambao pia ulifanyika mkoani Arusha mwezi Desemba mwaka Jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live