Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau TPA wasifu maboresho bandari Ziwa Victoria

9e73f0eacd6e7fc91c5db856834d9ef6.jpeg Wadau TPA wasifu maboresho bandari Ziwa Victoria

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wanaotumia bandari za Ziwa Vicrtoria wamepongeza uwekezaji na maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Walilieleza HabariLEO kuwa uwekezaji na maboresho vimeongeza ufanisi na kurahisisha shughuli za usafirishaji wa shehena za mizigo na abiria katika bandari hizo zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Wakala wa Forodha, Catherine Makalemo alisema vifaa vya kusafirisha mizigo kutoka ilipohifadhiwa hadi melini vimeongezeka hivyo kuwarahishia wateja kusafisha mizigo yao kwa urahisi katika Bandari ya Mwanza.

Wakala wa Forodha Mwanza, Peter Zakayo alimpompongeza Rais Samia kwa kuboresha bandari na kuipongeza TPA kwa kuondoa urasimu uliokuwa ukiwakwaza wafanyabiashara.

“Mama Samia amefungua milango kwa wafanyabishara na wawekezaji hata waliokuwa wameondoka sasa wamerudi, tunamuomba endelee kuboresha bandari zetu,” alisema.

Kutokana na vifaa kuongezeka, Zakayo alishauri taa ziongezwe katika Bandari ya Mwanza ili kuwezesha ufanyajikazi kwa saa 24.

Meneja wa boti ya MV Rafiki inayomilikiwa na kampuni ya Songoro Marine, Salehe Omar alisema maboresho yaliyofanywa katika Bandari ya Mwanza yamewezesha meli kuingia na kupaki vizuri bandarini tofauti na hapo awali.

Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Fransisco Mwanga alisema maboresho yaliyofanywa katika bandari hizo yameongeza tija na ufanisi, ambapo mwaka wa fedha 2020/2021 zimehudumia mizigo tani 172,422 sawa na asilimia 88 ya lengo la kuhudumia tani 195,200 na abiria waliohudumiwa ni milioni 425,151 lengo likiwa limevukwa kwa asilimia 169 la kuhudumia abiria 529,963 na vyombo vilivyohudumiwa ni 2,092 wakati lengo lilikuwa ni 1,091.

Mwanga alisema mwaka wa fedha 2021/2022 katika kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba, mizigo tani 175,400 sawa na asilimia 110 ilihudumiwa wakati lengo lilikuwa tani 91,434 na abiria waliohudumiwa ni 801,600 ambapo lengo lilivukwa kwa asilimia 114 ambalo lilikuwa ni abiria 374,950.

Mhandisi wa Bandari za Ziwa Victoria, Khamisi Mohamed alisema serikali imewekeza Sh bilioni 11. 24 kwa ajili ya kuboresha bandari zilizopo katika Ziwa Victoria.

Alisema maboresho yaliyofanywa ni ujenzi wa magati, ujenzi na uboreshaji wa majengo ya bandari, upanuzi wa majengo ya abiria katika bandari za Mwanza na Bukoba.

Kwa Mwanza alisema jengo limepanuliwa na kuwa na uwezo wa kuchukua abiria 400 kwa wakati mmoja tofauti na hapo awali lilipokuwa likichukua abiria 100, wakati kwa Bukoba kwa sasa linachukua abiria 450 badala ya 150 wa awali.

Alisema maboresho mengine ni ujenzi wa reli na madaraja yanayotumika kuingiza mabehewa ya treni ndani ya meli ambapo zaidi ya mabehewa 22 huingizwa ndani ya meli moja kwa muda mfupi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live