Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachuna ngozi waongezewa ujuzi

Mashimba Wachuna ngozi waongezewa ujuzi

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema wachuna ngozi za mifugo mbalimbali ya nyama nchini ili kuwaongezea ujuzi ikizingatiwa kwamba soko la ngozi ni sehemu ya biashara kubwa zainazoliingizia taifa kipato kikubwa.

Mashimba amesema hayo wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya Wizara hiyo chini ya Rais Samia Suluhu, jijii Dar es Salaam jana Machi 7, 2022.

“Jumla ya wachunaji ngozi 549 wamepatiwa mafunzo ya uchunaji bora wa ngozi kutoka katika mikoa nane ya kimkakati ya Mbeya, Geita, Mwanza, Singida, Tabora, Iringa, Manyara na Dodoma.

“Pia, Wakaguzi 40 wa ngozi wamepatiwa mafunzo ya ukaguzi wa ngozi kutoka katika Mikoa minne ya Arusha, Manyara, Mbeya na Kagera.

Vilevile, Wapanga Madaraja ya ngozi 67 wamepatiwa mafunzo ya uchambuzi na upangaji madaraja kutoka katika mikoa mitano ya kimkakati ya Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kagera.” Mashimba Ndaki, Waziri wa Mifugo na Uvuvi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live