Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji wadogo Mara kupewa maeneo yaliyofanyiwa utafiti

Madini Manganese Wachimbaji wadogo Mara kupewa maeneo yaliyofanyiwa utafiti

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Madini mkazi mkoa wa Mara Mhandisi Amin Msuya amewatoa hofu wachimbaji wadogo wa mkoa huo hasa walioko katika eneo la Nyamongo kuwa Wizara ya Madini inatarajia kutenga maeneo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyiwa utafiti lengo likiwa ni kuwasaidia wachimbaji hao kuachana na uchimbaji wa mazoea

Mhandisi Msuya ametoa kauli hiyo wakati wa kiliniki ya utatuzi wa migogoro hususani katika maeneo ya uchimbaji ambapo amesema wanaendelea kuongea na mgodi wa Barrick North Mara ilikuwapa fursa wachimbaji hao kuyatumia maeneo hayo ambapo pia itasaidia kuondoa yatizo la vijana wanaovamia katika mgodi huo

Katika hatua nyingine wachimbaji wadogo wametakiwa kuanzisha vikundi ambavyo vitasaidiwa na ofisi ya madini kuhakikisha vinafanya kazi katika mazingira bora na wezeshi ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kuongeza makusanyo kwa kuwa mkoa huo unashika nafasi ya pili katika makusanyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live