Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji madini wenye imani za kishirikina wanyooshewa kidole

49059 Wachimbajipic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema nia ya Serikali ni kuwahamisha wachimbaji wadogo wanaoamini ushirikina kwenye utafutaji wa madini kwenda katika utegemezi wa tafiti za kisayansi zinazofanywa na wataalam wa sekta hiyo.

Akizungumza leo Jumatano Machi 27, 2019 katika  uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Geolojia Nchini (GST), Biteko amesema taasisi hiyo imefanya utafiti katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema baada ya kutoa taarifa za tafiti katika baadhi ya maeneo kwa wachimbaji wadogo, walifanikiwa kupata madini waliyokuwa wakiyatafuta.

“Yale maeneo ambayo wametoa utafiti kwa wachimbaji wadogo kwa kweli wameenda kuchimba na kukuta resource (rasilimali) ipo. Hii ndio maana ya utafiti. Wachimbaji wetu tunataka kuwahamisha kwenye ule uchimbaji wa kwenda kwanza kupigiwa ramli kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata madini.

Mtu mmoja alisema kuna mahali wanatema mate kwenye kiganja akipiga upande yanayoelekea anajua mwamba unaelekea huko. Lazima tuwahamishe

wachimbaji wetu kutoka katika mfumo huo.”

Amesema pia alifanya ziara katika moja ya mikoa nchini (hakuutaja) ambao kabla ya kuchimba husafisha duara kwa kumwingiza mwanamke asiyevaa nguo katika shimo na kisha kuanza uchimbaji baada ya mtu huyo

kutoka.

“Lazima tuwahamishe wachimbaji kwenye uchimbaji wa namna hii. Na mtu pekee wa kuwahamisha hao so waziri wa madini bali ni taasisi yako mwenyekiti ya GST,’’ amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz