Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimba madini, wadau 100 waelekea China

Almasiii Madini Wachimba madini, wadau 100 waelekea China

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

wadau wa madini 100 wakiwemo wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa wameanza safari ya kwenda nchini China kwa ziara ya kujifunza.

Timu hiyo ambayo inahusisha wafanyabiashara wa madini na wataalamu kutoka Wizara ya Madini iliagwa rasmi jana, Agosti 11. Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, ambaye aliwataka kuhakikisha safari hiyo inaleta matunda.

Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Kampuni ya Touchbroad ya nchi hiyo imeandaa ziara ya wachimbaji kutoka Tanzania ili kuwawezesha kukutana na wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini China, kutembelea viwanda vya kutengeneza mitambo na vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji wa madini na kuwawezesha kupata uzoefu na wafanyabishara wa madini waliopo China na kupata teknolojia za uchimbaji na uchenjuaji

Chanzo: www.tanzaniaweb.live