Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wacheza kamari Tanzania mbioni kudhibitiwa

73147 KAMARI+PIC

Tue, 27 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bodi ya Michezo ya kubahatisha (TGB) inaandaa mkakati wa kubadilisha sheria na kuweka mfumo utakaowasajili wacheza michezo hiyo ili kuwadhibiti.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Agosti 27, 2019  jijini Dar es Salaam na mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo, James Mbalwe katika mafunzo ya wadau wa michezo ya kubahatisha.

Amesema licha ya kuwa michezo hiyo inaiingiza Serikali mapato ina madhara ya kiuchumi na kisaikolojia.

“Michezo ya kubahatisha ni burudani, lazima uwe na kipimo huwezi kuburudika tangu asubuhi hadi jioni,” amesema Mbalwe.

Amesema kuna sheria ya sasa inazuia tu watoto wasishiriki lakini sio watu wazima.

“Sheria yetu kwanza inakataza watoto tunataka kupanua wigo. Kwa mfano inaweza kuja familia ikasema mtu huyu amecheza sana, tunataka asiruhusiwe. kwa sasa hatuna sheria tunatumia uzoefu tu,” amesema.

Pia Soma

Amesema mbali na kubadilisha sheria, wataweka mfumo ambao wacheza kamari watajisajili ili kudhibitiwa.

“Mtu anaweza anaweza hata asiende kazini, akichukua mshahara anaumalizia huko, sasa wanaweza kuja mama au watoto wakasema baba asicheze. Tutakuweka kwenye mfumo, ukishafika tu mfumo unamkatalia.”

“Tunajaribu kujenga mtu yoyote kabla ya kucheza, utachukuliwa picha na majina yake kama umezuiliwa mfumo utakukataa. Kama umetibiwa unaweza kujitambua, utaruhusiwa,” amesema.

Mbalwe amesema changamoto iliyopo kwa wacheza michezo hiyo ni kukosa uelewa na kujikuta wakitumbukia kwenye uraibu.

“Kuna jambo linaendelea, kwa mfano mtu anasema watu wanaoshinda wanapendelewa au watu wengine wanajinyonga, lakini ukimwomba takwimu, hana.”

“Matatizo tunayopambana nayo pia ni uraibu, tutaandaa mafunzo kama haya ili watu wafahamu, kuna madhara makubwa ya michezo hii,” amesema.

Amesema Juni, 2019 sekta ya michezo hiyo ilichangia kodi ya Sh95 bilioni na imeajiri  watu  20,000.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz