Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabuni kadi za kieletroniki

N Card.png Wabuni kadi za kieletroniki

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: mwanachidigital

Katika jitihada za kupunguza makali ya mabadiliko ya tabia nchi, vijana wawili wametengeneza tekinolojia ya kidijitali inayosaidia kupunguza matumizi ya karatasi kwa ajili ya kutengeneza kadi za mialiko ya sherehe za kijamii hususani harusi.

Kadhalika, teknolojia hiyo inayotumia mfumo wa QR Code, inaelezwa kuwa itapunguza muda ambao wanafamilia wanautumia kusambaza kusambaza kadi za mialiko kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wanaishi katika maeneo tofauti tofauti.

Akizingumza mmoja wa wabunifu hao, Nderemo Muyaga, amesema kuwa karatasi huzalishwa kutokana na miti, na kwamba tekilojia yao inasaidia kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupunguza gharama kwa familia.

"Kwa miaka mingi utamaduni wa nchi nyingi za Kiafrika mualiko wa kuhudhuria shughuli mara zote hutolewa kwa njia ya kadi za karatasi, ni wachache wanaweza kuambiwa kwa simu na wakahudhuria, baada ya kuona hivyo, ndipo tukaja na wazo la tekinoljia hii rahisi ambayo ina faida nyingi," amesema.

Tekinolojia hiyo ambayo inajulikana ‘e-remmo’ waalikwa wanatumia kwenye simujanja na kwamba iko na QR code ambayo itamsadia mwalikwa ku-scani pale anapoingia ukumbini, huku wale wenye simu za kawaida wataingiza namba ya siri.

Chanzo: mwanachidigital