Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wataka kamati kunusuru biashara

Bunge Ed Wabunge wataka kamati kunusuru biashara

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Alitoa ushauri wake huo alipochangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26) uliowasilishwa bungeni jijini Dodoma juzi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

"Kitu kimoja kimenitia moyo lakini kimenisononesha sana. Tuna watu wazuri sana katika nchi hii katika mawazo ya kufanya biashara. Nimpongeze mpinzani wangu Mohamed Dewji ambaye tumesikia ameteuliwa na Rais wa South Africa kuwa mmoja wa watu ambao watamshauri," alisema.

Mbunge huyo alihoji kama Tanzania ina watu wa namna hiyo ambao nchi zingine zinawaona, serikali inawatumiaje watu hao.

Tarimba alisema serikali imezungumza mambo mengi katika mpango huo na hivyo ni lazima serikali itakapokuja kufanya majumuisho, ilieleze Bunge namna ilivyojitayarisha kuhakikisha kuwa inaitumia sekta binafsi.

Alisema sekta binafsi ni miongoni mwa wabia wakubwa katika mpango huo ambapo Sh. trilioni 40.6 zimeainishwa kuwa zitatokana na mchango wa sekta binafsi na Sh. trilioni 74.2 zitatokana na serikali.

Mbunge huyo alisema ni lazima jumuiya ya wafanyabiashara iangaliwe vizuri na angependa kuona mchango wa serikali katika kuhakikisha jumuiya hiyo inalelewa vizuri.

Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali (CCM), aliunga mkono hoja hiyo akisema Rais Samia ameanza vizuri kwa kushughulikia kero zilizokuwa zinawaumiza wananchi, lakini akatahadharisha kuwa bila kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara, fedha zitaendelea kutoonekana mifukoni mwa wananchi.

"Hakuna nchi inayoweza kukua kiuchumi bila kuwa na mazingira mazuri kwa wafanyabiashara. Hiki kinachosemwa fedha kutoonekana kwenye mifuko ya wananchi, ni matokeo ya biashara kuyumba.

"Mfanyabiashara asipopata faida, bidhaa za mfanyabiashara kama hazinunuliki, wanaoumia ni wananchi wa kipato cha chini kwa sababu wafanyabiashara hawatatoa fedha kuja huku chini.

"Kwa hiyo, kuna haja sasa serikali ikae na wafanyabiashara wakubwa hao kina Mo Dewji, izungumze nao ili kutatua kero zinazowakabili kwa lengo la kutengeneza mazingira mazuri ya biashara," alisema.

Mbunge wa Vunjo, Dk. Charles Kimei (CCM), aliitaka serikali kupunguza kukopa ndani ili kuepuka kudhoofisha taasisi za ndani kifedha.

Mtaalamu huyo wa masuala ya uchumi na fedha pia aliitaka serikali kuhakikisha kuwa kabla ya uzalishaji wa bidhaa za kilimo, ijiridhirishe juu ya soko la bidhaa husika.

Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu (CCM), alisifu hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini, akibainisha kuwa matokeo chanya yameonekana mjini Geita.

"Ukifika mjini Geita leo, utaona namna maendeleo yalivyopatikana kutokana na marekebisho ya sheria hii. Tatizo ninaloliona limebaki ni kutozingatiwa kwa sheria katika uingizaji wa malighafi kutoka nje," alisema.

Chanzo: ippmedia.com