Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge watahadharisha Ziwa Tanganyika kukosa meli

Wabunge Pic Tanganyika Wabunge watahadharisha Ziwa Tanganyika kukosa meli

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Wabunge wa Kanda ya Ziwa Tanganyika wameapa kuwa, hii ni bajeti yao ya mwisho kupitisha bila kuwa na meli katika ziwa hilo lakini zinazofuatwa ukanda mzima watapinga hata lije shinikizo.

Kauli hiyo imetolewa jana Mei 22, 2022 na wabunge wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka 2023/24.

Mwenyekiti wa Umoja wa wabunge hao ambaye ni Mbunge wa Kigoma (CCM), Kilumbe Ng’enda amesema uvumilivu kwao sasa basi kwani wamebaini kuwa, wenzao wa ukanda wa Ziwa Victoria waliungana na ndiyo maana ziwa hilo lina meli tano.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wabunge wa ukanda wa Ziwa Tanganyika tumeunda umoja wetu na mimi ndiye Mwenyekiti wao, tunasema hii ni mwisho na itakuwa mwisho kweli, lakini kwa bajeti ya mwakani tumejipanga na hatutamsikiliza mtu yeyote,” amesema Kilumbe.

Mbunge huyo amesema wenzao wa Kanda ya Ziwa Victoria waliposimama pamoja katika umoja wao, wamefanikiwa ndiyo maana wamekuwa na meli tano zinazofanya kazi wakati Ziwa Tanganyika hakuna meli hata moja.

“Tunasema na tunarudia kusema kuwa, mwakani hata akija nani kutushawishi hatutakuwa tayari kumsikiliza isipokuwa tunakuwa na msimamo wetu ame kuwe na meli zitakazokuwa majini,” amesisitiza.

Mbunge wa Kalambo (CCM), Josephat Kandege amependekeza ujenzi wa meli mbili ndogo badala ya kujenga moja kubwa ambayo kwa maelezo yake haitakuwa na tija wala maana yoyote.

Mbunge huyo amesema usafiri katika Ziwa Tanganyika ni kama kumesahaulika ukilinganisha na wenzao Ziwa Victoria hivyo akasema kwa umoja wao wanamuunga mkono Mbunge Kilumbe Ng’enda kwani ni ukweli hakuna meli Ziwa Tanganyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live