Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge washauri njia za kuongeza kasi uchumi

Wabunge Washauri Njia Za Kuongeza Kasi Uchumi Wabunge washauri njia za kuongeza kasi uchumi

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabunge wameishauri serikali izingatie kuboresha kilimo, elimu na mazingira ya biashara kama njia za kuongeza kasi ya kukuza uchumi.

Walisema hayo bungeni Dodoma wakati wakichangia mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo alisema ni muhimu kuzingatia mambo hayo wakati wa kuandaa dira mpya ya maendeleo ya 2025- 2050 sanjari na kujiuliza nchi zilizokuwa na uchumi sawa na Tanzania katika miaka ya 60’s zilifanya nini kufika zilipo sasa.

Profesa Muhongo alisema ili uchumi ukue kwa kati ya asilimia nane hadi 10, lazima kuboresha elimu katika ngazi zote, kuwe na nishati ya uhakika kwa bei nafuu, bidhaa bora na nyingi kupelekwa katika soko la dunia itakayokuwa na takribani watu bilioni 10 ifikapo mwaka 2050.

Alihimiza kilimo cha umwagiliaji mazao yenye soko kubwa duniani hasa mchele, ngano, viazi mviringo, mahindi, mihogo, maharage, soya, korosho na matunda.

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amehimiza serikali isikilize na itatue changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wakiwemo wa Kariakoo mkoani Dar es Salaam.

“Tukiiua Kariakoo tutakuja kushikana mashati humu ndani, Kariakoo ndio kila kitu kwa Tanzania kwa hiyo ni vizuri tupalinde…kamatakamata Kariakoo ni nyingi mno, hakuna mgeni anaenda kwenye nchi inayokamata, ukinunua katisheti unapini, ukinunua haka unapini..,” alisema Musukuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live