Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wanolewa Sheria ya Manunuzi ya Umma

Sheria Manunuzi Wabunge Wabunge wanolewa Sheria ya Manunuzi ya Umma

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), imetoa mafunzo kwa wabunge kuhusu Sheria ya Manunuzi ya Umma ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu.

Kwenye sheria hiyo ya mwaka 2011, wabunge walilalamikia kifungu cha 64 (k) kipengere cha pili ambacho kinatoa nafasi kwa makundi maalumu kushiriki fursa ya manunuzi ya umma.

Akizungumza leo Jumatano Juni 29, 2022 Spika wa Bunge, Dk Tulia Aksoni amesema, kundi la wanawake ni sehemu kubwa ya jamii hivyo, mafunzo hayo ni fursa ya kuwawezesha kusimamia na kuhakikisha utekelezaji madhubuti wa sheria hiyo unafanyika.

Dk Tulia amesema ni wajibu wa wabunge hasa wanawake kuipambania sheria ya manunuzi ya umma kwani ila taasisi ya umma inatakiwa kutenga asilimia 30 ya bajeti kuwezesha  makundi ya vijana, wanawake na wenye ulemavu.

"Mpango huu ni jitihada za Serikali kuwezesha makundi hayo kushiriki kwenye kukuza uchumi wa Taifa lao, ninyi wabunge ndiyo watu muhimu katika kupaza sauti za wahitaji," amesema Spika Dk Tulia.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la semina hiyo ni kuwawezesha wabunge hususan wanawake kuwa mstari wa mbele kwenye majimbo  yao katika kuelimisha juu ya umuhimu wa kutekeleza sheria hiyo.

Advertisement Waziri Dk Gwajima amesema wabunge wanawake wakiilewa vizuri sheria hiyo, itakuwa msaada mkubwa hata kwenye mabaraza ya madiwani na hivyo kuifanya jamii kufikiwa na elimu kwa uharaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TWCC, Mercy Silla  alisema  semina hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Samia Suluhu, ambapo aliwataka kuhakikisha kundi hilo la wawakilishi wa wananchi linafikiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live