Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wabaini sababu kukwama usindikaji wa maziwa Tanzania

58866 Pic+mawiwa

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imesema  kutoimarika kwa usindikaji wa maziwa nchini kunatokana na kukosekana kwa mazingira rafiki ya uwekezaji wenye tija ikiwa ni pamoja na wingi wa tozo na kodi zipatazo 28.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Mei 21, 2019 bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati hiyo, Mahamoud Mgimwa wakati akisoma maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020.

Amesema mazingira mengine yasiyo rafiki ni wingi wa taasisi za udhibiti na ukaguzi zipatazo 11  na miundombinu duni maeneo yanakozalishwa maziwa kwa wingi.

“Ushindani usio sawa baina ya wasindikaji nchini ambako wachakataji wa maziwa ya unga wamepewa punguzo ya kodi la asilimia 87.5 kuingiza maziwa ya unga nchini,” amesema.

Amesema changamoto hizo kwa kiasi kikubwa zinasababisha kuongezeka gharama za uwekezaji katika usindikaji na kushindwa kumudu ushindani wa bidhaa za maziwa zinazotoka nje ya nchi au kushindana na maziwa yanayozalishwa kutokana na maziwa ya unga yaliyopewa punguzo la kodi.

Kamati hiyo imeishauri mambo mbalimbali kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kujitathimini upya uamuzi wa kuweka kodi kwenye maziwa na bidhaa zinazotokana na maziwa ili kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT Exempt) kama ilivyokuwa kwenye sheria ya kodi ya mwaka 2012.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz