Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Tanzania wataka kuanzishwa kitengo cha kilimo hai

Wabunge Tanzania wataka kuanzishwa kitengo cha kilimo hai

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji nchini Tanzania, Mohamed Mgimwa ameitaka wizara ya kilimo nchini humo kuanzisha kitengo cha kilimo hai ili kuwanufaisha wakulima wengi wanaotumia kilimo hicho.

Mgimwa ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 27, 2019 wakati wa kongamano la kilimo hai jijini Dodoma lililowakutanisha wabunge, wakuu wa wilaya  pamoja na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali.

"Tunajua sera ya kilimo hai ipo lakini tunaambiwa haijafanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili, tunachotaka sisi kama wabunge tuambiwe sera hii inaanza kutekelezwa lini," amesema Mgimwa

"Tunaenda kwenye mabadiliko makubwa ya sheria ya kilimo na sera naamini Januari 2019 Serikali  itakuwa ni vyema kuangalia namna ya kuingiza sera hii na sheria yake ya kilimo hai," amesema Mgimwa

Naye Mkurugenzi msaidizi wa mazao, huduma za pembejeo na ushirika, Beatus Malema amesema Serikali ipo tayari kupokea changamoto zozote za wakulima wa kilimo hai kwani mazao yatokanayo na kilimo hai  yana fursa kubwa sana duniani.

"Nawashauri wakulima wanaozalisha mazao yao kwa kutumia kilimo hai waungane pamoja na serikali kwa kupitia vyama vya ushirika ili waweze kuwa wengi zaidi na kuongeza nguvu ya uzalishaji, upande wa serikali tuko tayari kupokea changamoto zenu na kuzifanyia kazi, "amesema Malem

Chanzo: mwananchi.co.tz