Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabulgaria kujenga hoteli Ngorongoro, Serengeti

05e702898349768a774097c20d2a44ca Wabulgaria kujenga hoteli Ngorongoro, Serengeti

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawekezaji kutoka nchini Bulgaria, wameonesha nia ya kuwekeza Tanzania kwa kujenga hoteli nne zenye hadhi ya nyota tano katika hifadhi za Taifa Serengeti, Ziwa Manyara na Tarangire na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana amesema kuwa hayo ni matunda ya filamu ya Royal Tour, ambayo imeanza kuvutia watalii na wawekezaji kutembelea nchini.

Dk Chana ameliambia bunge wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 bungeni mjini Dodoma leo Juni 3, 2022.

Pia wakala wa utalii zaidi ya 30 kutoka Marekani, Ufaransa na Lithuania wamehamasika kutembelea nchini, ili kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii kwa lengo la kuvitangaza katika nchi zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live