Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabainika kutumia leseni za kurithi

6e951776460a57413fbaccc01c413ef1.PNG Wabainika kutumia leseni za kurithi

Fri, 26 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADHI ya wafanyabiashara wa mifugo wamebainika kutumia leseni za kurithi za kusafirisha bidhaa hiyo kutoka kwa wazazi wao, kinyume na sheria zilizowekwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Brela, Andrew Mkapa alipozungumza na wafanyabiashara katika mnada wa Pugu, Dar es Salaam jana.

Alisema wafanyabiashara hao, wamekiri kutumia leseni za kurithi kutoka kwa wazazi wao walioawaachia biashara.

Alisema kufanya hivyo ni kinyume na kuwataka kubadilika na kukata leseni kwa wale walioachiwa biashara za kurithi upya kwa kuwa kuna taarifa muhimu zinahitajika kwa mhusika.

“Leseni za kurithi hazitakiwi, yule aliyeachiwa ni lazima akate ya kwake ndio maana wanaambiwa walete taarifa zao,”alisema.

Mkapa alisema wale wanaokwepa kufanya hivyo, wanaikosesha serikali mapato na kuwahimiza kuzingatia sheria ili wasije kuchukuliwa hatua.

Mmoja wa wafanyabiashara, Said Hamis aliwahimiza Brela kufungua ofisi kwenye mnada huo iwe rahisi kwa wafanyabiashara kukata leseni kwa kuwa wengi huishia mnadani hawaendi mjini.

Rajabu Mrisho alisema kitendo cha Brela kwenda kuwapa huduma katika mnada huo, kimewasaidia kupata kwa haraka leseni hizo, tofauti na wanapoomba wenyewe mitandaoni.

Ofisa Nyama kutoka Bodi ya Nyama, Edger Mamboi aliwashauri wafanyabiashara hao, kuhakikisha wanakidhi matakwa ya sheria zilizowekwa ili kutobughudhiwa.

Katika siku saba Brela ilizokaa kwenye mnada huo kwa ajili ya kutoa mafunzo ya umuhimu wa kukata leseni, imefanikiwa kutoa zaidi ya leseni 40 kwa wafanyabiashara wa mifugo.

Chanzo: habarileo.co.tz