Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandaaji wa maonesho wapewa angalizo

Anjella Kairuki SS Waandaaji wa maonesho wapewa angalizo

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amewataka waoneshaji wa onesho la Kimataifa la Swahili International Tourism Expo (Site) kuzingatia taaluma ili kufanikisha kuzielezea kwa ufasaha taasisi zao.

Akizungumza mkoani Dar es Salaa katika kikao cha maandalizi ya onesho hilo linalotarajiwa kuanza Oktoba 6, 2023 hadi Oktoba 8 ,2023 Waziri Kairuki amewataka waandaji wa onesho hilo kuwa na utaratibu wa kujiendeleza kupitia fursa za mafunzo kwa njia ya mtandao.

"Mtu anayekuwa kwenye banda lazima awe mzoefu, anayeaminika na awe anajua anafanya nini, lengo ni kuijenga sekta hii ya Utalii". Amesisitiza Waziri Kairuki

Naye Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amewataka waandaaji hao kuhakikisha wanaitangaza Tanzania kama nchi na sio taasisi mojamoja za wizara ya Maliasili na Utalii.

Onesho la Site litahudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika wakiwemo wanunuzi wa bidhaa za utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live