Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waagizwa kutumia Kaizen kuongeza tija

Cd3c4bc91da9cd5cc56f39bcde07f008 Waagizwa kutumia Kaizen kuongeza tija

Fri, 26 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WATUMISHI wa Wizara ya Viwanda wameshauriwa kutumia mafunzo ya KAIZEN katika kuongeza tija na ubora katika utendaji kazi na majukumu yao ya kila siku.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Dk Consolata Ishebabi wakati wa ufunguzi mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa wizara yaliyofanyika jijini hapa.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha watumishi wa wizara hiyo kubadili mtazamo, kuongeza tija, uwajibikaji na ubora mahala pa kazi.

"Tuiweke KAIZEN katika mipango yetu kuanzia ofisini hadi katika familia zetu ili kuongeza tija na ubora katika utendaji kazi na katika maisha yetu ya kila siku na tujipime kwa kutumia vipimo vya utumishi kama OPRAS,”alisema.

Mafunzo hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo "KAIZEN kwa Tanzania ya Viwanda Shindani kwa Maendeleo Shirikishi”.

Mradi wa KAIZEN unayofadhiliwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) unalenga kuongeza tija na ubora katika sekta ya viwanda na inaongozwa na misingi ambayo ipo katika ubunifu wa mawazo, maarifa na ushiriki wa kila mtu ndani ya taasisi, shirika au kampuni.

Mwaka 2019/2020 wizara hiyo ilifanya tathimini ya hali ya utekelezaji wa miradi ya KAIZEN na matokeo yalionesha kuwapo kwa ongezeko la ubora na tija kwa bidhaa za viwandani, hatua iliyochagizwa na usimamizi bora wa rasilimali watu, muda na miundombinu.

Chanzo: habarileo.co.tz