Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waagizwa huduma za fedha kuwafikia wakulima

7f9321f7f4a959fbbb4092f6230bdb81 Waagizwa huduma za fedha kuwafikia wakulima

Mon, 10 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa (pichani) amewaagiza mawaziri wa kilimo na wa fedha nchini kuhakikisha huduma za kifedha ambazo ni mahususi kwa ajili ya wakulima zinazotolewa na taasisi mbalimbali nchini ikiwemo huduma ya ‘NBC Shambani’ zinawa? kia wadau wa kilimo na kuwaletea tija kulingana na makusudio ya kuanzishwa kwake.

Waziri Mkuu alitoa wito huo mwishoni mwa wiki alipotembelea banda la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) lililopo kwenye Maonesho ya Kilimo maarufu Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Akiwa ameongazana na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wanaohusika na Kilimo; Uvuvi na Fedha, Majaliwa alisema kwa kiasi kikubwa amevutiwa na huduma mbalimbali za kibenki ambazo ni mahususi kwa ajili ya wadau wa kilimo, ikiwemo huduma mpya ya ‘NBC Shambani’ ambazo zikisimamiwa vizuri na wadau wote ikiwemo serikali zitaleta tija kubwa kwa walengwa na kuongeza uzalishaji na ukuaji wa uchumi.

“Ufanisi wa huduma hizi mahususi kwa ajili ya wakulima utaleta mwamko mkubwa kwao katika kufungua akaunti za kibenki, tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanashindwa kufanya hivyo kwa kuwa huduma hizo zilikuwa haziwagusi moja kwa moja.

Hivyo, pamoja na kuwapongeza Benki ya NBC nawaomba mawaziri msimamie hili kuhakikisha kweli huduma kama hii ‘NBC Shambani’ na nyingine huko zinawafikia wakulima kulingana na malengo ya kuanzishwa kwake,”aliagiza.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa tayari wizara hiyo ipo kwenye makubaliano na taasisi zote kubwa za kifedha nchini ikiwemo benki hiyo kuhakikisha wakulima wote wanakuwa na akaunti kwenye taasisi hizo ambazo hazitakuwa na makato kwao, hivyo huduma hiyo ya ‘NBC Shambani’ ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo muhimu.

“Lakini pia tulikubaliana AMCOS (vyama vya ushiri ka vya msingi vya wakulima) zote wanapopokea zile ‘AMCOS Fees’ waruhusiwe kutoa asilimia 50 ya hizo ada kwa ajili ya matumizi yao ila asilimia 50 ibaki kwenye akaunti zao kwa ajili ya kuendelea kuzalisha faida,”alifafanua.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kwenye banda la benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema mbali na huduma hiyo ya NBC Shambani pia benki hiyo kwa kushrikiana na wadau wengine ikiwemo Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake na Vijana (TABWA) pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) iliendesha mafunzo maalumu ya kilimo na biashara yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika maonesho hayo.

Akifafanua kuhusu huduma ya ‘NBC Shambani’, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa benki hiyo, Raymond Urassa alisema inalenga kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja.

Chanzo: habarileo.co.tz