Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waagizaji mafuta wakanusha upotoshaji unaosambazwa mitandaoni

Waagizaji Mafuta Wakanusha Upotoshaji Unaosambazwa Mitandaoni.jpeg Waagizaji mafuta wakanusha upotoshaji unaosambazwa mitandaoni

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa kimekaa kikao na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kuishia kwenye mtafaruku pamoja na kutokukubaliana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, TAOMAC haijakaa kikao na EWURA kwa zaidi ya wiki mbili, na pia haijawahi kuwa na mtafaruku na mamlaka hiyo.

Aidha, imesema sekta ya uagizaji na usambazaji wa mafuta kwa sasa inapitia changamoto ya ukosefu wa dola, lakini tayari imekaa vikao na mamlaka zinazohusika, na tayari imeahidiwa kuwa tatizo hilo linatafutiwa ufumbuzi.

“Wanachama wetu wanaendelea kuagiza mafuta, na wataendelea kufanya hivyo ili kuhakikisha nchi haikosi mafuta,” imesema taarifa iliyotolewa na TAOMAC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live