Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WRRB yatoa mafunzo mfumo wa stakabadhi ghalani

Stakabadhi Ghalaniii Ghalanii WRRB yatoa mafunzo mfumo wa stakabadhi ghalani

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala kama ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka kwa Watendaji wa kampuni za Waendesha ghala, Wasimamizi wa ghala, Meneja dhamana pamoja na washiriki binafsi.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Hashim Komba katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Komba alieleza kuwa Mafunzo haya yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa Wadau wote, vilevile ameitaka WRRB kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Pia, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Mary Fidelis.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala Asangye Bangu amesema kuwa lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi kwa kuzingatia sheria.

Aidha Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya hivyo, Washiriki waliojitokeza kupata mafunzo haya watapatiwa cheti cha kufuzu usimamizi wa shughuli za uendeshaji ghala ambacho kitatambuliwa na Bodi ya Stakabadhi za Ghala.

‘’nilipofanya ukaguzi nilibaini changamoto mbalimbali kwenye maghala, anaeshikiliwa kwanza ni Meneja na Mkurugenzi anakuwa hayupo ukimuuliza Mkurugenzi anakuambia Meneja wangu ndio anaehusika, kwahiyo mda mwingine unakuta meneja hana Taarifa, hivyo natoa wito kwa Washiriki wote kuzingatia Mafunzo yanayotolewa ili kuwaongezea uwezo wa Kiutendaji" Amesema Bangu -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live