Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WMA yawapigia chapuo wafanyabiashara wazalendo

WMA.jpeg Stella Kahwa, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, WMA

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Vipimo nchini (WMA) umesema kuwa unaendelea kutoa elimu kwa Wafanyabiashara wote nchini kutumia vipimo sahihi na ufungashaji bora wa bidhaa mbalimbali ili kuendana na masoko ya dunia katika upatikanaji wa bidhaa zilizo kwenye vipimo na ufungashaji bora kwa wananchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa maonesho ya Wafanyabishara wanawake yaliyoandaliwa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Stella Kahwa amesema wanatoa elimu kwa Wafanyabiashara hao kutumia vipimo sahihi na kufungasha sahihi ili kushindana katika Masoko ya ndani ya ndani na nje ya nchi.

Kahwa amesema kuwa Wajasiriamali wengi wanafungasha bidhaa zao kwa usahihi lakini kuna makosa madogo madogo ambayo yanaepukika ili kuwa na mafanikio katika ufungashaji wa bidhaa hizo zilizozalishwa.

"Sisi tuna tunahakikisha vipimo vipo sawa na bidhaa zinafungashwa kwa usahihi kwa Wajasiriamali waliopo kwenye Sekta ya biashara, tunaamini ukitumia vipimo ambavyo si sahihi, unaweza usifungashwe vizuri", amesema Kahwa.

Kwa upande wake, Miss Tourism, Angella Steven alipotembelea banda la WMA, amesema kuwa amejifunza mambo mengi ikiwa Wajasiriamali kupewa thamani katika bidhaa zao, sanjari na kutambua ushindani uliopo katika masoko mbalimbali ya ndani na nje.

"Nimejifunza pia, Wakala wa Vipimo wanavyorasimisha bidhaa za wajasiriamali wadogo kuwa kwenye njia rasmi ili kuepusha na biashara haramu na biashara ambazo zinapunja wananchi ambapo wananunua", amesema Anjella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live