Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WMA wapongeza masoko ya almasi, dhahabu

F9ea244eb522062c0595cc09b2e3d5e7.png WMA wapongeza masoko ya almasi, dhahabu

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKALA wa vipimo (WMA) mkoani Shinyanga imempongeza Rais John Magufuli kwa kuanzisha masoko ya ununuaji wa dhahabu na almasi kwa pamoja hali iliyowarahisishia kazi katika ukaguzi wa mizani.

Kaimu Meneja wa WMA mkoani Shinyanga, Hilolimus Mahundi, aliyasema hayo juzi katika ufunguzi wa Maonesho ya Kwanza ya Biashara na Teknolojia ya Madini

Mahundi alimshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuweka soko la madini na kuwawezesha kusimamia kwa urahisi suala la vipimo katika mizani wanazopimia dhahabu na almasi kubaini kama ziko sahihi kwa mujibu wa sheria ya vipimo.

Alisema hali hiyo imerahisisha na kusaidia juhudi zao katika kumlinda mlaji kupitia sekta ya biashara, mazingira, usalama na afya kwa kupitia vipimo sahihi.

"Sasa hivi hawa wauzaji wa madini wamepewa masharti ambayo ni pamoja na kwamba, leseni zao zinapokwisha muda ili kupata nyingine, lazima mzani wake uwe umethibitishwa na wakala wa vipimo hivyo, sheria inawabana," alisema.

Mahundi alisema sheria hiyo nayo imesaidia kuondoa upunjaji katika vipimo kwa ununuaji wa madini ya dhahabu na almasi kutokana na malalamiko yaliyokuwepo ya kutoaminiana.

Kwa mujibu wa Mahundi, wamekuwa wakisimamia bidhaa zilizo katika vifungashio ili kuwalinda wafanyabiashara na walaji katika maeneo hayo kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack, upimaji wa madini katika ununuaji unakwenda vizuri kwani hadi kufikia Julai mwaka huu, tayari kilo 752 zenye thamani ya Sh bilioni 42.5 zimenunuliwa.

Baadhi ya wanunuzi wa madini ya dhahabu na almasi waliofika katika maonesho hayo wakiwemo wauzaji kutoka kampuni ya Zahra, walikuwa wakionesha namna wanavyopima madini hayo katika mizani zao na kiasi cha pesa anachotakiwa kukipata muuzaji.

Chanzo: habarileo.co.tz