Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP yawanufaisha wakulima

Wakulima Pic Data WFP yawanufaisha wakulima

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walieleza hayo jana Jumanne Juni 7, 2022 wakati wakizungumza na wanahabari kuhusu manufaa ya mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu sekta hiyo, wakisema hatua hiyo imewasaidia kupata mahindi mengi yanayowatosheleza katika familia huku mengine wakiyauza kwa wadau mbalimbali.

"Nawashukuru WFP ambao walitujengea uwezo wa namna wa kuandaa eneo la kuvunia, kisha kutandika maturubai na kuweka mahindi baada ya kuvuna toka shambani.Hatua imesaidia mahindi kutoka katika hali ya ubora, pamoja kuhifadhi eneo salama.

"Zamani tulikuwa tukivuna tunayatupa chini, matokeo yake mahindi yanakuwa machafu na hayana ubora unaohitajika na wadau, matokeo yake tulikuwa tunaishia kula wenyewe na upotevu ulikuwa mwingi.Baada ya elimu hii nimefenikiwa kuvuna maguni nane katika shamba la ekari moja, lakini awali nilikuwa napata magunia matatu," amesema Mirambo Masoud.

Naye Zipora Mussa amesema katika mradi KJP shirika hilo, limetoa mashine za kupukuchia mahindi hatua iliyorahisisha mchakato tofauti na hapo awali walikuwa wakitumia mikono katika mchakato huo, hatua iliyofanya kuchukua muda mrefu.

Mkuu wa Programu za WFP wilayani Kasulu, Michael Bisama amesema mbali na kulisha wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu shirika hilo limejikita katika miradi ya kuwasaidia Watanzania katika wilaya zinazopokea wakimbizi ili kuhakikisha wananufaika kiuchumi.

" Tuliwafundisha namna ya uvunaji bora  na uhifadhi wa mazao yao kupitia vvyama msingi vya ushirika.Kasulu ni wakulima sana lakini ukihitaji tani tano za chakula  na ubora wa mazao sio rafiki ndio maana tuliwajengea uwezo katika eneo hili," amesema Bisama.

Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mji wa Kasulu, Dk Sudi Kundelya amelishukuru shirika hilo, halmashauri hiyo imekuwa mnufaika mkubwa wa KJP hasa namna walivyowajengea uwezo  na kuwaendeleza wakulima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live