Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP kunufaisha wakulima zaidi ya 200,000

Kilimo House WFP kunufaisha wakulima zaidi ya 200,000

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ZAIDI ya wakulima wadogo wadogo 200,000 wamenufaika na mnyororo wa thamani wa zao la mtama, alizeti na maharage katika Mikoa nane nchini.

Mratibu Mradi kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Willbroad Karugaba amesema hayo kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii wakati wa Maonesho ya 31 ya kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yaliyohitimishwa jana kwenye Viwanja vya Nanenane mkoani Dodoma.

WFP imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kutekeleza programu za kilimo na masoko zinazolenga zinazolenga kuboresha usalama wa chakula na kipato kwa wakulima wadogo kwa miaka 15 sasa.

"Kuanzia mwaka 2022 WFP imetanua wigo wake na kusaidia wakulima wadogo ambao wameongeza tija ya mazao na ziada kwa ajili ya soko, kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ambayo iliandaa miongozo ili kutoa elimu kwa wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo ili kupata mbegu bora.” Alisema.

Aidha alisema kuwa takwimu za hali ya chakula nchini zinaonesha kuwa uzalishaji wa mazao hayo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka lakini pia licha ya ongezeko hilo inakadiriwa kuwa asilimia 30 hadi 40 ya mazao hayo hupotea kila mwaka baada ya kuvuna.

Naye Mkulima kutoka Kijiji cha Ibwaga, Wilaya ya Kongwa mkoai Dodoma, Elizabeth Lenjima alisema amenufaika na WFP kwa kumuwezesha kupata mafunzo ya uzalishaji wa mbegu pamoja kudhibiti sumu kuvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live