Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WB: Vita vya Russia na Ukraine vitayumbisha uchumi wa dunia

Uchumi Mdororo Vita vya Russia na Ukraine vitayumbisha uchumi wa dunia

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Benki ya Dunia ameonya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unaweza kusababisha mdororo wa kiuchumi duniani - huku bei za vyakula, nishati na mbolea zikipanda.

David Malpass anasema nchi nyingi za Ulaya bado zinategemea sana Urusi kwa mafuta na gesi. Anasema hatua za Urusi kupunguza usambazaji wa gesi zinaweza kusababisha "kupungua kwa kiasi kikubwa" katika eneo hilo.

Anaongeza bei ya juu ya nishati tayari ina uzito kwa Ujerumani, moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Urusi na Ukraine ni baadhi ya wazalishaji wakubwa wa mbolea na chakula, na Malpass, akizungumza nchini Marekani jana, alisema nchi zinazoendelea tayari zimeathiriwa na uhaba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live