Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyanzo uhaba wa dola ni hivi hapa..

Fake Dolaaa Vyanzo uhaba wa dola ni hivi hapa..

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekiri uwepo wa upungufu wa fedha za kigeni hususani dola ya Marekani katika Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kunakochangiwa na uchumi kukabiliwa na athari za vita kati ya Urusi na Ukraine, covid-19, mabadiliko ya tabia Nchi na mabadiliko ya mwelekeo wa sera ya fedha katika kubaliana na ongezeko la mfumuko wa bei duniani.

“Athari za vita kati ya Urusi na Ukraine (na vikwazo kwa nchi ya Urusi) zilisababisha kuvurugika kwa mnyororo wa ugavi wa bidhaa na upungufu wa bidhaa duniani, hali hii ilipelekea kupanda kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hivyo mahitaji ya fedha za kigeni ya kununua bidhaa kutoka nje yaliongezeka hapa nchini na kuwepo kwa upungufu wa fedha za kigeni, hususani dola ya Marekani.

“Baada ya janga la Covid 19 kuisha, biashara na wekezaii duniani uliongezeka hali hii ilisababisha ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni katika Nchi nyingi, ikiwemo Tanzania, hivyo kupelekea kuwepo kwa upungufu wa dola ya Marekani”

“Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, hali hii inasababisha mafuriko, ukame na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi mbalimbali, hivyo kumekuwepo na ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni katika Nchi nyingi kukabiliana na hali hiyo, ikiwemo kujenga au kukarabati miundombinu” —— imeeleza taarifa ya BoT.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live