Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyanzo mbadala vya umeme vishushe gharama kuhamasisha viwanda

20579 PIC+UMEME TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miaka 13 ya matuimizi ya gesi asilia kutoka Songosongo katika kuzalisha umeme umesadia kuokoa zaidi ya Dola 5 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh11.6 trilioni) ambazo zingekutimika kuagiza mafuta kutoka nje.

Mpaka mwaka jana, takwimu za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) zinaonyesha zaidi ya Sh23.14 trilioni zimeokolewa tangu gesi asilia ilipoanza kutumika katika uzalishaji wa nishati na viwandani.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Songas, Nigel Whittaker anasema gesi asilia imepunguza gharama za uendeshaji na kuchochea uendeshaji wa viwanda.

“Kama Tanzania ina nia ya kuwa taifa la viwanda mwaka 2025, ni wakati muafaka wa kuwekeza zaidi katika gesi asilia ili kuigeuza ndoto hiyo kuwa kweli,” anasema Whittaker.

Songas ni kampuni tanzu ya Globeleq ya Uingereza, miongoni mwa wazalishaji wa umeme wa uhakika kwa bei nafuu ikiuza kwa wastani wa Sh135 kwa kilowati moja.

Kampuni Songas ambayo wanahisa wake wengine ni TPDC, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Tanzania Development Finance Company, huzalisha umeme kwa gharama ya Sh132 kwa kila kilowati.

Hii inaonyesha licha ya Songas kuongoza nchini kwa kuzalisha megawati 180 za umeme hata bei yake ni nafuu. Tanesco huuza kilowati moja kwa Sh270 kwa wateja wake hivyo kuhitaji vyanzo nafuu zaidi kwa ajili ya wananchi wengi wenye kipato cha chini.

Takwimu zinaonyesha Songas inasambaza asilimia 21 ya umeme kutoka kituo chake cha uzalishaji cha Ubungo Power Plant (UPP) na kuiuzia Tanesco. Kutokana na biashara hiyo, imepata faida ya Dola 554 milioni za Marekani (Sh1.2 trilioni) kati ya mwaka 2004 mpaka mwaka jana.

Licha ya kupunguza gharama za uzalishaji, takwimu za TPDC zinaonyesha mahitaji ya gesi asilia nchini yameongezeka mara mbili kutoka futi 145 milioni za ujazo kwa siku mwaka 2016 hadi futi 300 milioni mwaka uliopita.

Mapato ya Serikali kutokana na gesi asilia hasa kodi za tozo nyingine zinazolipwa na Songas iliyowekeza Dola 321.6 milioni (zaidi ya bilioni Sh726.8) yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60.

Uwekezaji

Gharama kubwa zimetumika kukarabati na kubadilisha mfumo wa uzalishaji kuruhusu matumizi ya gesi katika kituo cha UPP.

Upanuzi wa kituo cha UPP unakadiriwa kugharimu Dola 56.7 milioni (zaidi ya Sh128.1 bilioni) huku Kisiwa cha Songosongo (SSI) kikitumia Dola 125.6 milioni (Sh283.9 bilioni).

Uchimbiaji wa mabomba ardhini umegharimu Dola 52.1 milioni (Sh117.7 bilioni) na kuongeza ukubwa kutoka inchi 12 hadi 16 umetumia Dola 4.1 miloni (Sh9.3 bilioni).

“Kutokana na mahitaji ya umeme Tanzania, Songas inafanyakazi na watumiaji muhimu kutafuta fursa za kuboresha sekta ya nishati na ujenzi wa viwanda vinavyohitaji nishati nafuu,” anabainisha Whittaker.

Mkurugenzi huyo anasema Songas imeonyesha faida zake kwa Taifa na itaendelea kufanya hivyo katika siku zijazo. Kwanza, anasema kampuni inataka kukipanua kituo cha UPP kiwe na uwezo wa kuzalisha megawati 250 kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo nchini.

Upanuzi huo, anasema utafanyika ndani ya mwaka mmoja na utagharimu Dola 60 milioni (Sh137 bilioni).

“Tanesco itaamua kama itazalisha au la, lakini Songas lazima iendelee na mapato yetu hayatayumba,” Whittaker.

Kampuni hiyo ilianza kulipa gawio kwa wanahisa wake ikiwamo Serikali mwaka 2012 hadi mwaka jana ilikuwa imeshatoa zaidi ya Sh75 bilioni.

Kwa kutumia gesi ya akiba kutoka kisiwa cha Songosongo, tangu mwaka 2004 Songas imetengeneza ajira 72 za moja kwa moja kutokana na shughuli zake kutohitaji wafanyakazi wengi.

Kukabiliana na changamoto ya ujuzi uliopo katika soko la ajira kwa wafanyakazi wa sekta ya gesi, Whittaker anasema Songas hutoa mafunzo ya miezi sita kila mwaka kwa wahitimu sita wa vyuo vikuu. Kwa miaka sita sasa, program hiyo imewanufaisha wanafunzi 80.

Tanzania, ya pili kwa ukubwa kiuchumi Afrika Mashariki nakabiliwa na upungufu wa umeme kulinganisha na mahitaji yaliyopo hivyo kusababisha kukatika kwa nishati hiyo mara kwa mara hali iliyosababisha Serikali kutafuta vyanzo mbadala vya kuzalisha nishati hiyo.

Chanzo mbadala

Kaimu mkurugenzi wa TPDC, Kapuulya Musomba anasema gesi asilia inachangia kuzalisha nishati kwa uhakika hivyo kuhamasiha na kufanikisha maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi.

Anasema kwa kiasi kikubwa gesi asilia itapunguza utegemezi wa nchi kwenye mafuta mazito. “Kama hii itatokea, zaidi ya asilimia 55 ya umeme katika gridi ya Taifa utakuwa unazalishwa kwa gesi,” anasema Musomba.

Whittaker naye anasisitiza: “Hatuhitaji tena kutegemea maji kwani uhakika wake huathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Utayari wa Serikali

Whittaker anasema ili sekta ya umeme ifanikiwe, Serikali inapaswa kuhakikisha kunakuwa na sera ya wazi na kuweka mkakati wa kisheria kuondoa baadhi ya migongano iliyopo.

Anatoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kuwa haitakiwi kuripoti moja kwa moja wizarani. “Wazalishaji binafsi wa umeme (IPP) tunahitaji kuungwa mkono na Serikali). Si IPP wote ni hawafai. Baadhi yetu tuko vizuri,” anasema

Hata hivyo, Serikali imeandaa mwongozo wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ambao muda wowote utakapoidhinishw ana baraza la mawaziri utaanza kutumika.

Chanzo: mwananchi.co.tz