Arusha. Vyama vya ushirika vya akiba na mkopo zaidi ya 2,000 nchini Tanzania hatarini kufutwa kutokana na kutokuwa na anuani jambo ambalo linatia shaka kuanzishwa kwake.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 9, 2019 na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Tanzania, Tito Haule wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika wa akiba na mkopo.
Amesema vyama vya ushirika kwa sasa vipo 6,137 lakini zaidi ya 2,000 havifanyi kazi ipasavyo.
Haule amezitaka bodi kuhakikisha sheria za ushirika zinafuatwa, mikutano inafanyika kwa mujibu wa sheria kuhakikisha fedha za vyama vya ushirika zinalindwa.
"Kuna chama cha ushirika kilifanya vikao 25 kwa mwaka na kila kikao mshiriki analipwa Sh300,000 wakati sheria inasema vikao vifanyike mara nne kwa mwaka.”
“Na ikitokea dharura viongezwe viwili tu ili jumla viwe sita, lazima vyama vya ushirika vijue wakati wa mkutano," amesema Haule
Pia Soma
- Alichokisema Mbowe kuhusu Mwanakotide
- Majina wanafunzi watakaopata mkopo kutangazwa Oktoba 17
- Kuwasilisha kero, malalamiko Dar sasa kwa ujumbe wa simu ya mkononi
Willbard Gereki, mshiriki wa amesema kuwa mafunzo yamewapa uelewa na hakuna mwananchi atakaye omba mkopo akakosa kutokana na usimamizi mzuri wa serikali.